Vibaya Lyrics by Harmonize
"

Harmonize - Vibaya Lyrics


Oooh! Aaah! 
Oooh! Aaah!
Oooh! Aah!...
Oooh! Aah!...
Ooooh! Ooh!

Alisema mapenzi vita,
Mi na yeye tuungane kuwateketeza maadui 
[Eti Maadui]
Badala ya miezi kupita Aah! vikombe lazima vigongane
Na sio kwamba hayajui
[Eeh! hayajui]

Pigo za kusema vya ndani mi sinaga hizo
Ama kumtafuta mchawi ni nani ni kuongeza tatizo
Tuliapa, tutakuwa wa ndani hadi paradiso
Na tukatangaza peupe mambo hadharani na tatoo ndo hizo
Oh! Oh! Ooooh!
Sitaki kuamini kwamba, lile kapu la mabaya yangu
Halina hata machache mema
[Oh! Mema]
Nitakuwa mshamba, nikiyasema yote mabaya ya mwenzangu
Ili nionekane mwema

Japo mapenzi yanaumiza, I wish tusisemane (Vibaya vibaya)
Ili kesho tusizikane (Vibaya vibaya)
Usiwasikilize wapambe (Vibaya vibaya)
Wanachotaka maneno, ili kesho watuchambe (Vibaya vibaya)

Oooh! Aaah!
Oooh! Aaah!
Oooh! Aah!...
Oooh! Aah!...
Ooooh!

Nitunzie siri zangu
Nami nitunze zako za miaka rudi nenda
Kuna leo na kesho 

Mmmmh! Mmh!
Hata maadui zangu walikuwaga maadui zako
Hawawezi kukupenda wanakuvuta uwe kichekesho

Mmmmmh!
Maana hata ukisambaza
Picha zangu za aibu ni sawa, hata hunikomoi
Na hata utupu wako ukiutandaza
Kwa watu wangu wa karibu sio dawa, hujengi hubomoi

Mama kuna kamchezo mtunze mtoto wako
Na watu wenye majungu (Majungu)
Nilikubali kuviacha vya dezo
Sababu ya mapenzi yako, nikaachana na mzungu (Mzungu)

Maneno yao utadhani wanakutetea
Kumbe tudhalilishane wanachongojea
Usiwape faida wambea, na ni kama kawaida nakuombea

Sitaki kuamini kwamba
Lile kapu la mabaya yangu, halina hata machache mema 
[Ooh! Mema]
Nitakuwa mshamba, nikiyasema yote mabaya ya mwenzangu
Ili nionekane mwema

Japo mapenzi yanaumiza
I wish tusisemane (Vibaya vibaya)
Ooh! Lelee!
Ili kesho tusizikane (Vibaya vibaya)
Usiwasikilize wapambe (Vibaya vibaya)
Wanachotaka maneno ili kesho watuchambe (Vibaya vibaya)

Oooh! Aaah! Oooh! Aaah!
Oooh! Aah!...
Oooh! Aah!...
Ooooh! Ooh!

(Konde Music Worldwide)
B Boy thank you for the sound
Sound...
Sound…
"

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Contact Form