Rayvanny - Nyamaza Lyrics


Click on the image to download Rayvanny's music

 

"Rayvanny - Nyamaza Lyrics

Weka pombe sigara chini subiri tuongee

Zima kijiti marijuana za nini? Ngoja tuongee

Mbona ulisema mengi ukitaka nipotee?

Sa umefanya nini, na ulisema nini? wala usijitetee


Macho hayana pazia, nilimwona anavutia

Naye kanikubalia, kumbe moyoni unaumia


Dunia imejaa visanga, ubinadamu umekuwa majanga

Tembo amefungwa kwa banda, anataka kula kuku pia na vifaranga

Mungu tu akusamehe, wewe ni kama ndugu yangu

Upunguze maukali, uadui wa nini mwenzangu we


Ukitenda kosa na haujaomba radhi unakosea [Kosea]

Mama yake mzazi huruma ungemwonea [Mwonea]


Chunga kinywa kiwe na kituo, hekima ndio iwe funguo

Maneno ya nini? Unajivua nguo, kumbuka ulimwengu ni kama chuo


Click download Get Rayvanny Music


Ungenyamaza, [Kaa kimya]

Bora ungenyamaza [kama huna lamaana]

Ungenyamaza [ukikosa heshima]

Bora ungenyamaza [bora kukaa kimya]

Ungenyamaza [Aaah!] usiongee

Bora ungenyamaza [bora ungenyamaza]

Ungenyamaza tu, bora ungenyamaza [Kuwa muungwana]


Mmmmh! 

Hasira hasara

Mimi ni ndugu yako kanitoa kafara

Ukakesha hukutaka kulala

Ukipambana niharibikiwe kaka wa Mtwara


Ukasahau mapenzi ni siri, tena siri ya wawili

Kilichokuponza maadili, tamaa ukashindwa isitiri


Tunza heshima yako na mashabiki zako hadi mbungeni

Na unapotongoza warembo, boxer usiweke pembeni


Macho hayana pazia, nilimwona anavutia

Naye kanikubalia, kumbe moyoni unaumia


Ukitenda kosa na haujaomba radhi unakosea [Kosea]

Mama yake mzazi huruma ungemwonea [Mwonea]


Chunga kinywa kiwe na kituo, hekima ndio iwe funguo

Maneno ya nini? Unajivua nguo, kumbuka ulimwengu ni kama chuo


Ungenyamaza, [Kaa kimya]

Bora ungenyamaza [kama huna lamaana]

Ungenyamaza [ukikosa heshima]

Bora ungenyamaza [bora kukaa kimya]

Ungenyamaza [Aaah! usiongee?]

Bora ungenyamaza [bora ungenyamaza]

Ungenyamaza tu, bora ungenyamaza [Kuwa muungwana]"


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Contact Form