Basi Tu Lyrics by Lava Lava ft. Mbosso

Song: Basi Tu
Artist: Lava Lava Ft Mbosso
Licensed to YouTube by: Ngomma VAS (on behalf of Wcb Wasafi)

Basi Tu Lyrics by Lava Lava ft. Mbosso 

       
[Ayolizer]

Siku hizi hanipigii
Hata akikuta missed call zangu
Simu hashiki na akishika
Anauliza nani mwezangu

Mara anakata
Mara simu hewani haongei
Namaliza vocha
Anajizima data, eti amepanda bei
Kunifanya ndodocha

Eeeeeeh!
Najitumisha message
Mara mbili mbili
Anafungua anasoma
Majibu hayarudi eh! Eh! Eh!

Ila kwa Whatsapp page
Zaonyesha tiki mbili
Kujifanya hajaona
Ili mradi kusudi, na kunidharau

Ananiringia ringia [Nikoona] 
anajishebedu
Ananiringia ringia [hata nikimuita ati anani ….]
Siku hizi ananiringia ringia [ akiniona, anishebedu]
Ananiringia ringia [Eeeh! eh!]
Anajua nampenda [Basi tu]
Anafanya kusudi kuniumiza [Basi tu]
Ili mradi kuniliza [Basi tu]
Anafanya kusudi kuniumiza [Basi tu]
Ili mradi kuniliza

Aah! aah! aah! …

[Mbosso]

Na dhalia hainaga suu
Yaliyosemwaga ya kale
Kufurahia kunguru nafuu
Wakigombana mbalale

Moyo unawaka moto kifuu
Yanichoma maumivu mshale
Enyi malaika mlio juu
Shusheni amani itawale

Nayamaliza madhehebu
Kusomewa madua
Mbolea imekausha mbegu
Imeshindwa chipua

Mtazame nampenda kwa sana
Leo a-n-a nifanya mi nalia
Ina maa-na ndo nime-cho-kwama
Au jama-a sina fungu kwenye dunia

Najitumisha message
Mara mbili mbili
Anafungua anasoma
Majibu hayarudi

Ila kwa Whatsapp page
Zaonyesha tiki mbili
Kujifanya hajaona
Ili mradi kusudi na kunidharau

Ananiringia ringia [Ananiringia]
Ananiringia ringia [Ananidengulia]
Siku hizi ananiringia ringia
Anairusha rusha roho yangu
Ananiringia ringia Eeh! Eh!

Anajua nampenda [Basi tu]
Anafanya kusudi kuniumiza [Basi tu]
Ili mradi kuniliza [Ila basi tu]
Anafanya kusudi kuniumiza [Basi tu]
Ili mradi, ila nenda

Nenda mwambie asante [nenda umwambie] 
Mwambie asante [Aah!] 
Nenda mwambie asante [asante Sana]
Mwambie asante [Ooh! mwambie]
[Mimeshukuru sana]

Nenda mwambie asante [kanifunza maumivu]
Mwambie asante [nilikuwa siyajui]
Nenda mwambie asante
Mwambie asante [Ustahimilivu nisilipize uadui]

[Kwa Mix Lizer]

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Contact Form