Wale Wale Lyrics by Lava Lava


From The #PromiseEp​ 
Track No.1 Wale Wale

Wale Wale Lyrics by Lava Lava


Aaah!
Aaaah!

Naumwa nina maradhi
Nipelekeni hospitalini
Mwenzenu naumwa moyo umekufa ganzi
Nimechoka kunywa quinini

Nahisi ukichaa
Nusu tahira uchizi
Naona kinyamazongo
Niliyavagaa rambi nikaipiga mbizi
Ikanipasua ubongo (Ubongo)

Angeniambia basi, tungeachana kizungu
Ningempa nafasi, kuliko kutupanga mafungu
Nisinge gasi, japo ni ngumu machungu
Chanya na hasi, anapanganga Mungu

Kibatari kazidisha tambi, penzi limelipuka
Ye anacheat haogopi dhambi, anaruka ruka
Moyo kaupiga bambi, umeshateuka
Popote anaweka kambi, kutwa nachepuka

Yaani ndo wale wale
Wanaokujaga na tafadhali nakupenda (Wale wale)
Wakimaliza shida zao wanakwenda (Ndo wale wale)
Ati Ooh! nilipotoka nilitendwa (Wale wale)
Kumbe ni waongo, waongo

Oooh! nenda mwambie
Mapenzi hayana jangili yanaumiza
Tena mwambie
Kuna walo matajiri washalizwa

Usimfiche mwambie
Mapenzi hayana utabiri si miujiza
Fanya mwambie
Mimi si wa kwanza kuumizwa

Yaliwatesa vikongwe
Tulisoma vitabuni
Nami amenipa mazonge
Najikaza kisabuni

Sawa mimi ni mnyonge
Damu yangu ya kunguni
Mi fungu la tatu kibonda
Mwezangu lake kumi

Angeniambia basi, tungeachana kizungu
Ningempa nafasi, kuliko kutupanga mafungu
Nisinge gasi, japo ni ngumu machungu
Chanya na hasi, yote napanganga Mungu

Kibatari kazidisha tambi, penzi limelipuka
Ye anacheat haogopi dhambi, anaruka ruka
Moyo kaupiga bambi, umeshateuka
Popote anaweka kambi, kutwa nachepuka

Yaani ndo wale wale
Wanaokujaga na tafadhali nakupenda (Wale wale)
Wakimaliza shida zao wanakwenda (Ndo wale wale)
Ati Ooh! nilipotoka nilitendwa (Wale wale)
Kumbe ni waongo, waongo

Mwache afanye anachotaka (Hanikomoi, wala hanikomoi)
Sishtuki hata (Hanikomoi, wala hanikomoi)
Sina hofu sina mashaka (Hanikomoi, wala hanikomoi)
Bure anatapa tapa (Hanikomoi, wala hanikomoi)

(The Mix Killer)Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Contact Form